search

.

Monday, 15 October 2012

YANGA KAMBINI KESHO

Kikosi kamili cha mabingwa wa soka Afrika Mashariki na Kati Yanga, kinatarajia kuingia kambini hii leo katika hoteli ya  Up Lands iliyopo Changanyikeni jijini Dar  kwa ajili ya kujiandaa na michezo yake ya ligi kuu soka Tanzania Bara.
 
Akizungumza na HABARI TANZANIA mapema leo mmoja wa viongozi  wa timu hiyo kongwe hapa nchini alisema kuwa  wameamua kuingia kambini mapema  ili wajiandae kupata ushindi kwenye mchezo unaokuja  dhidi ya Ruvu Shooting na pia michezo mingine.
 
"Ndiyo tunaingia kambini kesho, kujiwinda na mchezo unaofuata, lengo likiwa ni kupata  ushindi", alisema kiongozi huyo. 
 
katika hatua nyingine kiongozi huyo amesema kuwa  majeruhi  Kevin Yondani na Said Bahanuzi, wako kwenye hali nzuri na  wataakuwa kambini hapo  kwa  mazoezi mepesi na  baadae wataingia kwenye  mazoezi muhimu.
 

0 comments: