Subscribe:

search

.

Wednesday 17 October 2012

ZAMBI ATWAA UENYEKITI WA CCM MBEYA


Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya.
Zambi kapata kura 888  na kufuatiwa na Allan Mwaigaga ambaye amepata kura 318 na kufuatiwa na Reginald Msomba aliyepata kura 237


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima ndiye alikuwa msimazi wa uchaguzi huu akitangaza matokeo


Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mstaafu mkoa wa Mbeya, Nawab Mullah, akimkaribisha mwenyekiti mpya Mh Zambi

Allan Mwaigaga ambaye amepata kura 318 na kuwa mshidi wa pili akiwashukuru wanachama wa ccm katika uchaguzi huo na kusema sasa makudi yavunjwe maadam mshindi kapatikana 


Reginald Msomba aliyepata kura 237. mshindi wa tatu nae pia akiwashukuru wanachama wa ccm katika uwanja wa sokoine jijini mbeya

Mkuu wa mkoa Mbeya Abasi Kandoro kulia katikati  chales Mwakipesile kushoto kabisa mwenyekiti mstaafu mulla wakiwa makini kufuatilia matokeo uwanjani hapo  mida ya saa sita kamili usiku

wanachama wa ccm wakiwa makini kusikiliza matokeo uwanjani hapo



Mwenyekiti mpya Zambi akipongezwa na mwenyekiti mstaafu Mullah mara baada ya kutangazwa mshindi

Baadhi ya wanachama wa ccm wakimvisha mwenyekiti wao mpya mashada ya maua


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima akimsisitizia jambo fulani mwenyekiti mpya wa ccm mkoa wa mbeya G. Zambi


Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mashariki Godfrey Zambi amabaye sasa ni mwenyekiti wa ccm mkoa wa Mbeya akiwashukuru wanachama wa chama hicho kwa kumchagua

0 comments: