Subscribe:

search

.

Wednesday 10 October 2012

AFISA UHAMIJI ANUSURIKA KIFO MWANZA

Habari zilizotufikia muda mchache uliopita zimebainisha kwamba Ofisa wa Uhamiaji katika Ofisi ya Mkoa wa Mwanza, Albert Buchafwe amenusurika kuuawa kwa risasi baada ya kushambuliwa na Mkuu Msaidizi wa Kituo cha Polisi cha Nyakato, Abubakar Zebo kwa madai kuwa walikuwa wakilishambulia jambazi moja
Akisimulia kisa hicho Ofisa huyo Buchafwe amesema baada ya kuwashiwa taa na gari la ofisa huyo wa polisi alisimama na kujitambulisha akiwa ndani ya gari, lakini aliamriwa kuzima taa za gari lake na kutoka ndani ya gari lake. “Nilitii nikazima taa, lakini nilisita kutoka katika gari langu, nilijitambulisha kwamba mimi ni ofisa uhamiaji na kumtaja jina ofisa huyo, ambaye aliendelea kunilazimisha kushuka ndani ya gari huku nikiona akijiandaa kunishambulia kwa bastola yake,” amesema Buchafwe.
Lakini taarifa nyingine kutoka katika mitandao ya kijamii, zinasema wakati ofisa uhamiaji huyo akijiandaa kushuka huku akijitambulisha, askari mwenye sare za polisi alishuka huku akiwa na SGM na haraka Buchafwe alilazimika kugeuza gari na kukimbia huku gari lake likishambuliwa kwa nyuma kwa zaidi ya risasi tano.
Mbali na hilo Buchafwe amesema kuwa anatilia shaka tukio hilo kwa kuwa askari huyo kwa kuwa ana uhusiano wa karibu na mke wake ambaye wamekuwa na ugomvi na ofisa huyo wa polisi kwa muda mrefu sasa. Ofisa huyo wa uhamiaji amesema kutokana na ugomvi huo ametalakiana na mkewe mahakamani na kwamba tukio hilo alikuwa la bahati mbaya bali la mamaksudi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,

Liberatus Barlow amesema tukio hilo limetokea jana saa 4: 13 usiku wakati ofisa wa uhamiaji alipokuwa akirejea nyumbani kwake na kukutana na gari dogo aina ya Suzuki lililomuashia taa likimuashiria kusimama. Kamanda Barlow amesema tukio hilo lilitokea bahati mbaya baada ya kuwapo kwa majambazi katika eneo hilo.

0 comments: