Subscribe:

search

.

Wednesday 10 October 2012

FUKWE ZAFUNGWA KUHOFIA NYANGUMI WEUPE

Sehemu kubwa ya pwani ya Afrika Kusini imefungwa kufuatia mzoga wa nyangumi mwenye ukubwa wa mita 30 kusukumwa na maji pembezoni mwa fukwe na kuanza kushambuliwa na jamii ya papa weupe.
Mzoga wa nyangumi huyo umelazimika kuondolewa haraka ufukweni ulikokuwa ukielea, kwa kuwa ulikuwa ukifukuziwa na papa weupe kadhaa walio ugeuza kitoweo na kuhatarisha maisha ya watu.
Mamlaka husika zimechukua hatua ya kuuondoa mzoga huo lakini pia imefunga mtandao wa fukwe hizo kuanzia Muizenberg hadi Monwabisi kwa tahadhari.
Mzoga wa Nyangumi ukipimwa urefu.

Mashine Maalum ya kubebea vitu vizito kama Makontena ikifanya kazi ya kusomba mzoga huo.


Jitihada za kumbeba Nyangumi huyo kwa kutumia mashine maalum za kubebea makontena zikiendelea.
Nyangumi akiwa tayari amepakiwa kwenye Lori.
Safari imeanza ya kumsafirisha Nyangumi huyo sehemu kunakohusika.

0 comments: