search

.

Monday, 8 October 2012

SUMAYE AWEKA WAZI KUTOKUWA NA NIA YA KUKATA RUFAA

Mhe. Sumaye akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

Waziri mkuu mstaafu Mheshimiwa Fredrick Sumaye ameeleza kusikitishwa na kutoa tahadhari juu ya kukithiri kwa rushwa ya mtandao ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika maeneo mbalimbali yenye chaguzi ambapo mtu hutoa fedha ili watakaochaguliwa wawe wafuasi wake mbele ya safari .


Sumaye akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema pia kuwa ndoto za wanaodhani kwamba atahama CCM kwenda chama kingine, ni sawa na fisi anayevizia mkono wa mtu akidhani utakatika lakini asiambulie kitu, “Napenda kueleza wazi kwamba, sina nia wala ndoto ya kuhama CCM kwenda Chama chochote, mimi sipo CCM kwa sababu ya cheo”, alisema.

Akizungumzia kushindwa kwake ujumbe wa NEC katika uchaguzi wa Hanang, Sumaye amedai rushwa imesababisha kuanguka kwake. Katika uchaguzi huo, ambao ni miongozi mwa chaguzi za CCM zinazoendelea nchini kote katika nafasi mbalimbali, Dkt. Mary Nagu aliibuka mshindi.

0 comments: