Subscribe:

search

.

Wednesday 17 October 2012

WANANCHI WAGOMEA MKUTANO MBEYA



WANANCHI wa Kata ya Nsalaga katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, wamegoma kufanya mkutano wakimshinikiza mkurugenzi wa jiji hilo kumrejesha aliyekuwa ofisa mtendaji wa kata hiyo, Chripian Matola, aliyehamishiwa Kata ya Maendeleo ili kujibu tuhuma zinazomkabili
 Matola anadaiwa kutumia kinyume cha sheria fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Uyole zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa shule hiyo.
Walisema ofisa mtendaji aliyeondoka alikuwa hajasoma mapato na matumizi kwa takriban miaka miwili iliyopita na kuna fedha za ujenzi wa Shule ya Sekondari Uyole zilikuwa hazijatolewa taarifa, hivyo isingekuwa rahisi kwa ofisa mtendaji mpya kujibu maswali ya wananchi.
  “Ndugu mwenyekiti, kuna upotevu hapa wa zaidi ya shilingi milioni tatu ambazo hatujui mtendaji wetu aliyeondoka alizifanyia nini. Tume iliundwa na kuchunguza sasa leo mnatusomea nini hatutaki …..tunamhitaji yeye aje asome mwenyewe tumuulize maswali,” alisema Jerry Mwakipesile.
Kutokana na hali hiyo, Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Diwani wa kata hiyo, Timoth Mandondo (CHADEMA), alilazimika kuahirisha mkutano na kuwaahidi wananchi kupeleka maombi yao panapohusika.

0 comments: